News & Reports‎ > ‎

Untitled Post

posted Feb 24, 2021, 2:08 AM by William Ombade
KATIKA HOSPITALI YETU KAMA TARATIBU YETU TUNAENDANA NA KALENDA YA LITURJIANA VIPINDI VYA MWAKA WA KANISA  KWA HIYO KWA SASA  TUKO KWENYE KIPINDI CHA KWARESIMA AMBAPO KILA IJUMAA TUNAENDA KWENYE NJIA YA MSALABA 2021

NJIA YA MSALABA

Tufwate njia ya msalaba, . Tuifuwate, mpaka Kalvario. Tusimamepo, bila haya. Msalaba, Msalaba uponya roho.

Sala mbele ya Altare.

Ee Mkombozi wangu, ninakuja Leo kufuata njia ile uliyoshika siku ya kufa sadaka yetu. Nimetubu dhambi zangu zote; ninataka kugeuza mwendo wangu, ninaomba kwako niwapatie roho za waumini marehemu waliomo toharani, rehema zote zilozotolewa na kanisa kwa Njia ya Msalaba.

Nawe Maria Bikira Mtakatifu, uliyefuata njia ile nyuma ya mwanao Yesu, uniangalie kwa wema, unitie moyo mkuu, nisipende dhambi tena, nikivumilia kàzi na usumbufu na mateso na matukio yatakayonipata.

Umekosa nini we Yesu, Kushitakiwa bure kwa Pilato, Wenye kustahili hukumu, Si wewe, si wewe Bwana ni sisi.

KITUO CHA KWANZA.

Yesu anahukumiwa afe.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.

-Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Pilato anamhukumu Yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa Wayahudi. Anabembeleza urafiki wa Kaysari.

Ee Yesu usiye na kosa, hata Mimi ningeweza kutenda mema mengi, lakini

naogopa macho ya wezangu, na maneno yao. Ee Bwana, uniima-rishe utashi Wangu, nijitegemee katika kushika madaraka yangu.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

K.Ee Bwana, Utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Ole mslaba huo mzito, Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu. Mwiliwe waenea mateso. Alipa, alipa madhambi yetu.

KITUO CHA PILI.

Yes anapokea msalaba.

-Ee Yesu, tunakuabudu, tunakushuru.

-Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.

Yesu anakubali kuelemewa na msalaba kwa ajili ya wokovu wa watu. Ndivyo anavyonifundisha moyo wa sadaka, moyo wa kujitolea na kujisahau kwa ya wengine.

Ee Yesu wangu mkarimu, mimi pia ninao msalaba wangu; jirani zangu, mwezangu wa ndoa, watoto, wazazi wangu, kazi zangu, joto, baridi, njaa, kiu, vishawishi, magonjwa na matatizo mengine ya maisha, wajibu wangu kwa Mungu, kwa Umma na kwa Kanisa, Hayo yote in msalaba. Unipe ukarimu wako ee Yesu, niyapokee bila ya kunung'unika, na kuyabeba vema.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukizwe Baba na....

K.Ee Bwana, Utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Ona muumba mbingu na nchi yupo chini mzingo wamwelemea na mtu kiumbe chake kwa ukali Ampiga, ampiga bila huruma

KITUO CHA TATU.

Yes anaanguka mara ya kwanza.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru

-Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Yesu amedhoofika sana, anaanguka chini, kisha anasimama, anaendelea na safari ya ukombozi.

Ee Yesu uliyeanguka chini ya msalaba kwa ajili ya udhaifu, ukasimama tena; usiache katika Tamaa nikianguka dhambini, Bali nisimame Mara moja, nikufuate.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Huko njiani we Maria waonaje hali ya mwanao Ni damu tupu na vidonda Machozi, machozi yafumba macho.

KITUO CHA NNE.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru

-Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Wote wawili mama na mwanawe wanaumia moyoni kwa ajili ya dhambi zangu.

Ee Yesu, Mwana wa Maria, unitilie moyoni mwangu upendo na Ibada kwa Bikira Maria, unijalie na ulinzi wake, nisitende dhambi tena.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Kwa simon heri ya kweli Mimi pia Yesu nisaidie kuchukua mzigo wa ukombozi Kuteswa, kuteswa pamoja naye.

KITUO CHA TANO.

Simoni wa Kirene anamsaidia Yesu.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.

-Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.

Nausifu ukarimu wa Simon wa Kirene. We Bwana, unijalie ukarimu kama huo, nitie ushujaa kama huo, niitikie nami wito wa kukusadia kuchukua msalaba.

Nitoe zaka na michango yote ya uenezaji wa dini; nijitolee mimi mwenyewe katika kazi ya maendeleo ya dini. Uwajalie vijana wengi wito wa upadre, waweze kuchukua msalaba pamoja nawe kwa ajili ya wokovu wa dunia. Uwaimalishe viongozi was dini. Usitawishe moyoni mwa waumi wote mwamko wa utume.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukizwe Baba na....

K.We Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Uso wa Yesu malaika Betlehemu walikuabudu Bahati yake Veronika Kupangusa, kupangusa mfalme was mbingu.

KITUO CHA SITA.

-Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru

-Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Mama huyu ni kinyume kabisa cha pilato. Veronika anajua analopaswa kutenda, na analitenda bila kujali macho na maneno ya makundi ya watu waovu.

Ee Yesu, ulihemtuza Veronika zawadi ya picha ya uso wako juu ya kitambaa, unijalie ushupavu na ujasiri wake wa kutenda mema, ili roho yangu ipambwe kwa chapa ya uungwana na utakatifu wako.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Wakimvuta huku na huku Wauaji wanamchokesha bure Chini wamtupa bado kwa nguvu Aibu, aibu yao milele.

KITUO CHA SABA.

Yesu anaanguka Mara ya pili.

-Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru

-Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu uliyelegea mno kwa mateso makali, unapoanguka mara ya pili kwa ajili ya udhaifu wa mwili, wanionya kwamba hata Mimi naweza kurudi dhambini kwa udhaifu wa moyo.

Nipe basi neema ya kuepuka nafasi za dhambi na visa vyenye kunikwaza na kurudisha dhambini.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Wanawake wa Israeli Musilie kwa sababu hiyo Muwalilie hao kwa dhambi Upanga, upanga ni juu yao.

KITUO CHA NANE.

Akina mama wanamlilia Yesu.

-Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru

- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Asanteni sana akina mama kwa moyo wenu wa huruma.

Ee Yesu uliyetulizwa na wanawake, unripe moyo wa kuwaheshimu akina mama wote. Uwaite na wasichana wengi waingie utawa, ili watulize Moyo wako Mtakatifu kwa sala na sadaka zao.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, kwa amani. Amina.

Mwokozi sasa ni ya tatu Waanguka chini ya msalaba Katika dhambi za uregevu Nijue, nijue kutubu hima.

KITUO CHA TISA.

Yesu anaanguka mara tatu.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru

-Kwa kuwa umewakomboa with kwa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu unayezidi kudhoofika kwa mateso unaanguka mara ya tatu, upate Kunistahilia neema ya kuutiisha mwili Wangu name kuusulibisha, licha ya kuepuka nafasi za dhambi.

Mara ngingi mno ninajibovusha kwa kupenda mno starehe, na tafrija. Ee Yes .wema, nisaidie kuufuata mfano wa mtakatifu Paulo, niutese mwili wangu na kuutumikisha, ili nipate siku moja tuzo mbinguni.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhumie...................W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Muje malaika wa mbingu Funikeni mwiliwe kwa huruma Vidonda vyake na utupu Askari, askari wamemvua.

KITUO CHA KUMI.

Yesu anavuliwa nguo.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru

- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.

Askari wanamvua kwa nguvu nguo yake, iliyogandamana na madonda yake; wanaamsha mara moja mateso yote aliyoteswa tangu .wanzo.

Ee Yesu, unayavumilia mateso makali haya, upate kunifundisha kuuvua kwa nguvu moyoni mwangu urafiki mbaya, au kitu kingine cho chote kile kinachoharibu urafiki wa Mungu, hata ikinipasa kutoa sadaka kubwa.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani. Amina.

Hapo mkristu ushike moyo Bwana wako alazwa msalabani Mara miguu na mikono Yafungwa, yafungwa kwa misumari.

KITUO CHA KUMI NA MOJA.

Yesu anasulibishwa msalabani.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushuru

-Kwa kuwa umewakomboa kwa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu uliyepigiliwa misumari msalabani, nakutolea akili na utashi wangu, vifhngwe pamoja na miguu yako, nipate kuwaza, kusema na kutenda siku zote yale tu yanayolingana na utukufu wa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu, mimi ni mfungwa wako. Nisadie kuimarisha kifungo hicho kwa sala, sakramenti na fadhila za kikristu.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Yesu mpenzi nakuabudu Msalabani unapohangaika Nchi yatetemeka kwa hofu Na jua, na jua linafifia.

KITUO CHA KUMI NA MBILI.

Yesu anakufa msalabani.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru

-Kwa kuw umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.

Ee Yesu uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, unijalie niichukie dhambi, nisiishi kamwe katika dhambi.

Nifahamu kwamba nilipobatizwa kwa jina lako, nilibatizwa katika mauti yako, ili utu wangu wa kale usulibishwe nawe, mwili wa dhambi uangamizwe, nisitumikie tena dhambi.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Mama Maria mtakatifu Upokee maiti ya mwanao Tumemwua kwa dhambi zetu Twatubu, twatubu kwake na kwako.

KITUO CHA KUMI NA TATU.

Yesu anashushwa msalabani.

Ee Yesu, uliyeshushwa msalabani baada ya kufa, unijalie nidumu katika maisha ya kujitoa sadaka mpaka siku ya kufa kwangu.

Nielewe na nikubali kwamba baada ya kufa ndiyo mwisho wa vita na mashindano ya kikristu.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Amina.

Pamoja nawe kaburini Zika dhambi na ubaya wa moyo Yesu tuwe wakristu kweli Twakupa, twakupa saaa mapendo.

KITUO CHA KUMI NA NNE.

Yesu anazikwa kaburini.

Ee Yesu, ulizikwa kaburini, ukafufuka siku ya tatu. Mimi pia nilizikwa pamoja nawe kwa njia ya ubatizo katika mauti yako.

Kwa vile wewe ulifufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, unijalie nami nifufuke, yaani nishike mwenendo mpya, mwenendo wa uzima wa neema.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Katika roho yangu Bwana Chora mateso niliyokutesa Nisiyasahau madeni Na kazi, na kazi ya kuokoka.

-Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukiru

-Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Habari njema aliyotuletea Yesu no kwamba baada ya ijumaa kuu huja sikukuu ya Pasaka: kwamba punje yake; Bali ikifa, hutoa mazao mengi.

Twakushukuru, we Yesu, kwa mateso yako, lakini twakushukuru hasa kwa ufufuko wako, kwa kuwa huo ufufuko ndio unaotupa hakika ya kuwa hatuzaliwa kwa ajili ya mateso na maumivu, bali kwa ajili ya heri ya milele.

Baba yetu..................

Salamu Maria...........

Atukuzwe Baba na...

K.Ee Bwana, utuhurumie...............

W.Utuhurumie..........

Roho za waumini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

 

SALA YA MWISHO

Mbele ya altare: Yesu wangu, kwa uchungu wote uloona juu ya msalaba, na kwa kuzimia kwako kwa ukali wa mateso, unijalie nguvu ya kuvumilia kwa moyo taabu zote sasa na saa ya kuzimia kwangu.

Nawe Maria Mamangu. Kwa uchungu wrote ambao moyo wako umejaa ulipomnwona Mwanao mpenzi kuinama kichwa na kuzimia, unifadhili nife kifo chema.

 

Comments