News & Reports‎ > ‎

Sala ya Jubilei ya Miaka 50 ya Hospitali ya Wasso

posted Dec 2, 2009, 10:23 AM by Unknown user   [ updated Sep 3, 2014, 9:45 PM by Dr Angela Meipuki ]

Sala ya Jubilei ya Miaka 50

Ya Hospitali ya Wasso

 

Ee Yesu, ulipotembea ulimwenguni wagonjwa wa kila aina walikukimbilia wakiwa na matumaini thabiti, kwamba watapata msaada na kupona. Wewe hukumkataa hata mmoja, uliwapokea wote katika upendo wako mkuu wa kimungu. Wanfunzi wako uliwatuma waponye wagonjwa na kuwahurumia wenye ulemavu, wawe mabalozi wa upendo wa Mungu na waweke ishara za wokovu wa milele katika huduma kwa wale wanaoteseka.

Tunashukuru kwa miaka 50 ya Hospitali ya Wasso, ambayo ni mahali pa kukimbilia kwa wale wanaoteswa na maradhi na magonjwa. Tunashukuru kwa wale wote, ambao walijitolea katika hopitali hii kwa binadamu wagonjwa na wenye ulemavu, katika uuguzi na udaktari na tiba, katika kujenga hospitali na kuitunza, katika kuiendeleza katika changamoto zote. Tunashukuru kwa wafadhili wengi, ambao walifungua mioyo yao kuwasaidia maskini kwa kupitia hospitali hii.

Tunakuomba: Uibariki hospitali yetu iweze kuendelea kutoa huduma ya uuguzi na udaktari wa kisasa, uwabariki wafanyakazi wake wawe na nia nzuri ya kujitolea kwa wenzao wagonjwa, na uwabariki wagonjwa wote wapate kupona nafsi, roho na mwili.

AMINA!

 

(Imetungwa na Thomas Brei, kwa tarehe 2/9/2014)

Comments